Klabu ya Everton imetangaza rasmi kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Marco Silva ikiwa ni miezi 18 tu kuwa na klabu hiyo kufuatia kipigo cha 5-2 walichokipata dhidi ya Liverpool ugenini katika uwanja wa Anfield usiku wa December 4 2019.
Uongozi wa Everton umechukua maamuzi hayo kufuatia kuona timu yao inazidi kuyumba hadi sasa ikiwa imecheza micheza 15 ya EPL wakiishia kushika nafasi ya 18 katika Ligi Kuu England inayoshirikisha jumla ya timu 20.
Katika michezo hiyo 15 Everton ikiwa chini ya utawala wa kocha Marco Silva wameshinda game 4, sare mechi 2 na wamepoteza mechi 9 wakiwa na pointI 11.
Kwa sasa mshambuliaji wa zamani Duncan Ferguson amekuwa msimamizi wa muda na ataiogoza klabu hiyo dhidi ya Chelsea siku Jumamosi.
Friday, December 6, 2019
Everton yamtimua kocha wake Marco Silva
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment