Bruno Tarimo maarufu kama 'Vifuaviwili' bondia wa ngumi za kulipwa amesema kuwa siri kubwa ya kupata ushindi mbele ya bondia Nathaniel May raia wa Australia ni kujituma bila kukata tamaa.
Pambano hilo la raundi 10 la uzito wa kg 59 lililofanyika Ijumaa nchini Sydney lilikuwa ni la kuwania mkanda wa International Super Featherweight Defense (IBF) ambao ameutwaa Vifuaviwili baada ya kushinda kwa pointi.
Vifuaviwili alisema kuwa alijipanga kupeperusha bendera ya Tanzania akiwa ugenini jambo ambalo lilifanikiwa kujibu kwa kupata ushindi. Vifuaviwili ameweka rekodi nzuri kwa Tanzania kwa upande wa ngumi kimataifa akicheza jumla ya mapambano 28 amepoteza pambano moja kwa pointi na akishinda jumla ya mapambano 27.
Tuesday, December 10, 2019
Bondia Bruno ataja siri ya kumtwanga Nathaniel May
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment