Adbox

Friday, December 6, 2019

Arsenal bado yaandamwa na Jinamizi baya

Klabu ya Arsenal licha ya kumfukuza kocha wake Unai Emery kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo mfululizo yasiyofaa, Arsenal bado haijakaa sawa na imeendelea kuutafuta ushindi kwa shida katika michezo yake mbalimbali.

Arsenal wakiwa nyumbani usiku wa Disemba 5 2019 walikuwa wenyeji wa Brighton katika mchezo wao wa 15 wa EPL msimu huu, licha ya sapoti kubwa ya mashabiki Arsenal wamepoteza kwa kufungwa magoli 2-1.

 Magoli ya Brighton yakifungwa na Adam Webster dakika ya 36 na Neal Maupay dakika ya 80, huku goli pekee la Arsenal likifungwa na Lacazette dakika ya 51 ya mchezo huo ambao uliifanya Arsenal ishuke hadi nafasi ya 10 katika EPL kwa kuwa na pointi 19 na Brighton wakipanda hadi nafasi ya 13 kwa kuwa na point 18.

Game hiyo inaiingiza Arsenal katika rekodi mbaya Ulaya kwa kuwa ndio timu pekee katika timu zinazotoka Ligi 5 kubwa Ulaya msimu huu, kuruhusu kupigiwa mashuti mengi 52 (On Target) kuliko timu yoyote, hiyo imetokea baada ya Brighton kupiga mashuti 9 (On target).

No comments:

Post a Comment

Adbox