Adbox

Wednesday, November 27, 2019

Wapangaji NHC kuhakikiwa

Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameliagiza shirika la Nyumba Tanzania -NHC kupitia upya mikataba walioingia kwa ubia na taasisi binafsi ili kuangalia namna serikali inavyoweza kunufaika kutokana na mikataba hiyo.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya NHC iliyopo Jijini Dar es salaam na kuitaka bodi ya shirika hilo kupitia upya mikataba 192 waliyoingia katika miradi ya ubia baina yao na watu binafsi

Aidha waziri Lukuvi ameiagiza bodi hiyo kupitia mikataba ya wapangaji wote walipo katika Nyumba za Shirika hilo na kujiridhisha kama wanaoishi katika Nyumba hizo ni wapangaji halali.

Waziri Lukuvi ametumia fursa hiyo kulipongeza shirika la Nyumba Tanzania kwa kuanza kutekeleza miradi yake kwa kutumia fedha za ndani za Shirika badala ya kwenda kukopa katika benki za biashara.

No comments:

Post a Comment

Adbox