Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama leo, Jumanne Novemba, 26 atatangaza utaratibu mpya wa kununua nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar Es Salaam.
Akiongea mara baada ya kumaliza kukagua mradi huo wa nyumba zinazomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), jana Jumatatu Novemba 25, Waziri Mhagama amebainisha kuwa atatoa utaratibu huo mpya wa namna ya kununua nyumba hizo zilizo wazi ili wananchi waweze kunufaika kwa kupata makazi bora na salama.
Mfuko huo wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na umeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2018, Jukumu kuu likiwa ni kukusanya michango na kulipa mafao ya kustaafu kwa watumishi wa umma.
Tuesday, November 26, 2019
Utaratibu wa kununua nyumba za bei nafuu kutangazwa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment