Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kuna mwananchi wa Msamvu amesema kazi yake ni kupiga debe sasa hayo madebe yakiisha atapiga nini?
Rais Magufuli amehoji leo akiongea na wananchi wa Msamvu, Morogoro akiwa njiani akielekea mkoani Dodoma.
"Kuna mmoja hapa amesema kazi yake ni kupiga debe tu, sasa madebe yakiisha atapiga nini? maana ya kupiga debe anapiga milango ya magari lakini magari hayo yana dereva na kondakta kwanini unakwenda kupiga gari la mwenzako? lazima tuambizane ukweli" amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli ametoa pole kwa ajili ya wananchi waliopata ajali ya moto mkoani humo huku akisema kama ni mbinu za shetani zishindwe.
Wednesday, November 20, 2019
Unapiga debe, Madebe yakiisha utapiga nini? - Rais Magufuli
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment