Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano imeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 38.4 zilizotakiwa kutumika kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa 43,200 nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma za matibabu ya upasuaji wa kibingwa.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface na kuongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano, Taasisi hiyo imeendelea kuimarisha na kuboresha huduma mbalimbali za afya kwa wananchi.
Dkt. Respicious anasema kutokana na maboresho na kuimarika kwa huduma ya afya, Taasisi ya MOI ndani ya kipindi cha miaka minne imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 43,200 waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania wengi na pesa za Serikali ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
"Gharama za matibabu za wagonjwa hao kwa ndani ya nchi zilikuwa Tsh Bilioni 16.5 na kama wagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu, jumla ya Tsh Bilioni 54.9 zingetumika, na hivyo kuifanya taasisi kuokoa kiasi cha Tsh Bilioni 38.4 ambazo zitatumika kwa shughuli nyingine za maendeleo."
Aliongeza kuwa Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne iliyopita imeweza kupokea kiasi cha Tsh. Bilioni 16.5 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo jengo jipya la MOI pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa ambavyo vimeweza kuleta mageuzi na maboresho ya huduma za afya katika Taasisi hiyo.
Akitolea mfano, Dkt. Respicious anasema katika fedha hizo zilizotolewa na Serikali, taasisi hiyo iliweza kuongeza idadi ya vitanda kutoka 150 hadi 350 kwa wagonjwa wa kawaida, na kufanya kutowepo na mgongjwa anayelala chini kwa sasa, sambamba na kuongeza idadi ya vitanda kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum kutoka vitanda 8 hadi 18.
Saturday, November 23, 2019
Taasisi ya MOI yaokoa Bilioni 38.4 matibabu Nje ya Nchi
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment