Msanii wa muziki, AliKiba amesema hawezi kushiriki kwenye tamasha la Diamond Platnumz kwa sababu na yeye anatafuta mafanikio na hana ugomvi na msanii huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kiba amesema, “Ninamuheshimu kwa namna anavyoutangaza muziki, lakini siwezi kutumbuiza kwenye tamasha lake kwa sababu na mimi natafuta mafanikio yangu, ”amesema Kiba.
Amesema atafanya ziara aliyoiita ‘Unforgatable’ nchini nzima akiweka kambi za kupima afya kila mkoa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Kiba amelazimika kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo mara ya pili, wiki iliyopita Diamond alisema uongozi wa lebo ya WCB unafanya mazungumzo na Kiba ili akatumbuize kwenye tamasha la Wasafi Festival linalofanyika leo kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Saturday, November 9, 2019
Siwezi kuhudhuria tamasha la Diamond - AliKiba
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment