Rais John Magufuli ambaye yuko njiani kuelekea Shinyanga amewaahidi wananchi wa Shelui walioomba Kituo cha Afya kuwa wavumilivu na ifikapo Januari Serikali itawasilisha shilingi milioni 250 tayari kwa kujenga kituo hicho.
Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo baada ya mwananchi mmoja kumuomba Rais kusaidia ujenzi huo ulioshindwa kutekelezeka kwa takribani miaka 15 huku akikumbusha ahadi ya Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete aliyoitoa ya kuwapelekea shilingi milioni 200.
Akijibu ombi hilo, Magufuli amesema, aahidi ya Rais mstaafu ni aahidi ya Serikali hivyo ataitekeleza na kuongeza milioni 50 katika aahidi hiyo huku akiwataka watakaoshinda zabuni hiyo kutekeleza ujenzi huo kwa uaminifu na haraka kwa uwepo wa huduma za afya katika eneo hilo ni muhimu.
"Aahidi ya Rais Kikwete, mimi nitatekeleza kama kijana wake ambaye pia aliniamini na kuteua katika nafasi mbalimbali, lakini suala la parking (maegesho) hilo nawaachia halmashauri, mbunge wenu, diwani wenu na ninakubaliana nanyi ni jambo zuri litawasaidia pia kupata mapato.." amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli katika eneo hilo pia alielezwa umuhimu wa kuwepo kwa kituo cha afya na maegesho kwa madai kuwa eneo hilo limekuwa na idadi kubwa ya watu sambamba na kupokea majeruhi wengi kufuatia eneo hilo kuwa karibu na mlima Sekenke ambao umekuwa ukisababisha ajali mara kwa mara.
Wednesday, November 27, 2019
Rais Magufuli aahidi kutekeleza ahadi ya Kikwete
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment