Adbox

Wednesday, November 27, 2019

Ndugu zangu vya bure hakuna, sikuja kuleta hela - Rais Magufuli

Rais John Magufuli amesema hakuna vya bure kwa wasiotaka kufanya kazi na kuwataka watu kuacha kulalamika hawana hela wakati hawajitumi.

Ametoa kauli hiyo Mkoani Tabora leo baada ya Mwananchi mmoja kulalamika Maisha magumu.

“Vya bure vimeisha na bado vitaisha zaidi, Ndugu zangu vya bure hakuna hata mimi sina vya bure, wewe unataka mkono wako uwe soft haufanyi kazi halafu unataka hela, mimi sikuja kuleta hela mfukoni mwako, nimekuja kuwaambia ukweli fanyeni kazi, sio kulalamika tu” alisema Rais Magufuli.

Mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Abel Mpinga, mkazi wa Wilaya ya Igunga mbele ya Rais John Magufuli alisema,"Maisha ni magumu fedha hakuna watu wana hali mbaya akina mama wananyang’anywa televisheni, friji kwa ajili ya mikopo. Tunaomba mheshimiwa tuachie fedha mengine yote hatuna tatizo na wewe,”

No comments:

Post a Comment

Adbox