Kasi ndogo ya ukusanyaji mapato ya Kodi ya pango la ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro imemsononesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ta Makazi, Dkt. Angeline Mabula na kuagiza halmashauri hiyo kuongeza kasi ili kufikia lengo la mapato ya kodi ya ardhi.
Akiwa katika ziara yake ya siku moja katika wilaya hiyo Dkt Mabula aligundua kuwa halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka 2018/2019 imekusanya shilingi milioni 12.3 na mwaka huu kufikia Novemba imekusanya milioni 10 ya kiwango ilichopangiwa cha milioni 55.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, kiwango hicho cha makusanyo katika halmashauri ya Gairo ni kidogo na hakijafikia hata nusu ya makadirio ya shilingi milioni 55 iliyowekewa halmashauri hiyo kukusanya kwa mwaka na makadirio hayo hayalingani na uhalisia wa makusanyo ya halmashauri.
Aliitaka halmashauri ya Gairo kupitia idara yake ya ardhi kuongeza kasi ya makusanyo ya maduhuli ya kodi ya pango la ardhi kwa kuwa kodi hiyo ndiyo inayoisaidia serikali kutekeleza miradi mikubwa aliyoieleza kuwa mingi inataegemea kodi ya ndani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe amemuahidi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa ofisi yake itayafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa ikiwemo uandaaji wa Mpango Kabambe katika wilaya hiyo iweze kupangika kimji sambamba na kuwa na Mji wa Serikali utakaojumuisha taasisi zote za serikali zilizopo katika wilaya hiyo.
Thursday, November 21, 2019
Naibu Waziri Mabula akerwa na makusanyo ya kodi ya ardhi Gairo
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment