Adbox

Friday, November 22, 2019

Mahakama yataja tarehe ya kusomwa Hukumu ya Malinzi na wenzake watatu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itatoa hukumu dhidi ya Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi na wenzake watatu December 05 mwaka huu, Malinzi Na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na utakatishaji fedha .

Hakimu Mkazi Mkuu Huruma shaidi amesema kesi hiyo haijakamilika na itasomwa tarehe iliyopangwa, awali kesi hiyo ilisikilizwa na Hakimu Mkazi Maira Msonde lakini kwa sasa amehamishwa kituo cha kazi

Mbali na Malinzi Watuhumiwa wengine ni aliyekuwa katibu Mkuu TFF Mwesigwa, Mhasibu TFF, Mwanga na Karani Flora Rauya, wataendelea kukaa Mahabusu mpaka tarehe ya kusikilizwa kesi.

No comments:

Post a Comment

Adbox