Adbox

Tuesday, November 19, 2019

Katibu Mkuu CCM apokea maoni, mapendekezo ya wanachama wao Tawi la China

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dk. Bashiru Ally Kakurwa amepokea taarifa ya maoni na mapendekezo ya wanachama wa CCM Tawi la China yaliyowasilishwa na Katibu wa Tawi hilo Ndugu Yazidi Iddi katika ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi, Dodoma.

Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wanachama wake, makundi mbalimbali katika jamii ambayo yatazingatiwa katika uandishi wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya 2020-2025.

Ndugu Yazidi Iddi ametoa salamu za pongezi kutoka kwa wanachama wa CCM wanaoishi miji mbalimbi katika nchi ya China kwa Viongozi wa Chama na Serikali. Wakipongeza juhudi za dhati zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi kuisimamia Serikali ili kuhakikisha nchi yetu inapiga hatua za maendeleo kwa kasi na kuwa nchi ya mfano barani Afrika.

Uchumi wetu umeendelea kuimarika kutokana na usimamiaji mzuri na madhubuti wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2015-2020 kupitia Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano chini ya Ndugu John Pombe Joseph Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndugu Ali Mohamed Shein.

Katibu Mkuu amewataka wanaCCM na watanzania waliopo nchini China kuwa mabalozi wazuri wa nchi yetu na kujiepusha na vitendo vya kihalifu. Amewahimiza kutumia fursa zilizopo China katika kuchangia maendeleo ya uchumi, taaluma na jamii hapa nchini.

Katibu Mkuu amewataka watanzania wanaoishi China kudumisha upendo, umoja na mshikamano miongoni mwao na kudumisha urafiki wa kihistoria baina ya watu wa mataifa yetu.

No comments:

Post a Comment

Adbox