Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameiunga mkono kauli ya Wazee wa CCM wa Wilaya ya Kusini Unguja ya kuwa Wilaya hiyo itaendelea kuwa ngome ya CCM.
Dk. Shein aliyasema hayo katika ukumbi wa Skuli ya Kizimkazi Mkunguni, Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipofanya mazungumzo na Wazee wa Wilaya ya hiyo.
Makamo Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar alieleza kuwa Wilaya ya Kusini Unguja ina historia kubwa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo, anaamini kuwa Wilaya hiyo ina uwezekano mkubwa wa kuendelea kuwa ngome ya chama hicho.
Alieleza kuwa ushindi wa CCM katika chaguzi zake zote ni jambo ambalo halina mbadala kwani hilo ni agizo la Katiba ya Chama hicho kutokana na malengo iliyojiwekea.
Alisema kuwa malengo ya CCM yako wazi kwamba chama hicho kimeundwa kwa lengo la kushinda uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Aidha, aliwataka viongozi wote wale ambao wako madarakani na wale wasiokuwepo madarakani bado wana nafasi ya kukipigania Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama wanavyofanya Wazee na Mabaraza yao pamoja na Jumuiya za Chama hicho.
Thursday, November 21, 2019
Dk. Shein aunga mkono kauli ya Wazee wa CCM
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment