Na.Amiri kilagalila-Njombe
Wakulima wa mazao aina mbili ya mpunga na mahindi nchini kuanza kunufaika na bima mazao kutokana na kukabiliwa na hasara kubwa pindi zinapotokea changamoto katika uzalishaji wa mazao hayo.
Miongoni mwa mikoa inayoanza kunufaika na bima ya mazao hayo hapa nchini ni pamoja mikoa ya Ruvuma kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Songea na Madaba,mkoa wa Njombe kwa upande halmashauri ya wilaya ya Njombe na Ludewa pamoja na Mkoa wa Morogoro kwa upande wa halmashauri ya Kilombero na Mvomero kutokana na kupatikana kwa wakulima wengi katika maeneo hayo.
Akizungumza na Muungwana Blog baada ya uzinduzi wa bima hiyo uliofanyika katika kijiji cha Mtwango kilichopo wilayani Njombe,Joshua Ongaga meneja mradi wa bima ya mazao (WEKU) alisema bima hiyo itaanza kupatikana katika mikoa hiyo kwa wasambazaji wote wa pembejeo pamoja na vyama vya wakulima kwa kuanza na wakulima wadogo wanao lima shamba lenye ukubwa wa nusu ekari au chini ya ekari moja.
“Tofauti na aina zingine za bima ya mazao,bima ya kilimo ya lima salama,wakulima wataweza kuinunua moja kwa moja kutoka katika vyama vyao katika mfumo wa kadi scratch cards,hivyo wakulima wana uwezo wa kutumia simu zao za mkononi kwa kusajili bima zao huku kadi moja ya bima ikiuzwa kwa gharama ta Tsh 5,000 na ikilinda ghalama ya uzalishaji yenye thamani ya Tsh 70,000 tu,tunatarajia wakulima wawekeze kwa uhakika kwamba mkulima akiingia shambani awe na uhakika wa matokeo wa yale aliyoyawekeza”anasema Joshua Ongaga
Consolatha Gabone ni meneja mamlaka ya usimamizi wa bima nyanda za juu kusini,anasema bima ya kilimo kwa sasa ni muhimu kwa kuwa serikali kwa sasa inahamasisha kilimo cha biashara hivyo ni lazima wakulima kuwa na bima kutokana na changamoto zilizopo katika kilimo.
“Bima ya mkulima ni kitu muhimu sana na serikali yetu sasa hivi inataka kilimo cha biashara kinachoweza kumkwamua mkulima,haiwezekani kufikia ndoto bila ya kuwa na bima kwasababu kilimo kina changamoto kubwa sana kama hali ya hewa,wadudu,kukosa soko hivyo kuna mambo mengi yanaokinga ndoto ya mkulima kufikiwa”anasema Consola Gabone.
Afisa kilimo wa mkoa wa Njombe Wilson Joel anawaasa wakulima wa mkoa wa Njombe kuipata elimu vizuri juu ya bima kutoka kwa wataalamu waliopo ili kuondo changamoto wanazoweza kukutana nazo wakati wa matumizi ya bima.
“Najua mwitikioa ni mkubwa hivyo wakati wa kutoa elimu utakapofika kutoka kwa hawa wadau wetu,ninachotaka kuwaasa wananchi kuwa karibu na kulewa vizuri kwasababu usipoelewa vizuri na ukachukuwa kitu na kuweza kuanza kulalamika na sisi kama serikali kwa kushirikiana na wadau tumeshalileta kwenu”anasema afisa kilimo Wilson Joel.
Naye afisa kilimo kutoka mkoa wa Ruvuma Adrew Tarimo aliwataka aliwataka wanaume kutumia pesa katika bima badala ya kucheza michezo ya kubahatisha huku afisa kilimo kutoka mkoa wa Morogoro Peter Gama akiwaomba wakulima kuwatumia vizuri wataalamu wa kilimo katika changamoto zozote.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Jeritha Mligo ambaye ni afisa kilimo wilaya hiyo alisema zipo changamoto nyingi ikiwemo ukame na mvua za mawe zinazotokea bila taarifa hivyo ni wajibu kwa wakulima kuchangamkia fursa hiyo.
“Kuna changamoto za mvua za mawe,ukame na vinaweza kutokea bila kutarajia sasa vitu kama hivi vinatakiwa kuwa na bima ili uweze kufidiwa,hivyo rai yangu kwa wakulima kuchangamkia fursa hii”anasema Jeritha Mligo
Joyce Kaduma na Christopher kiliwa ni baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mtwango walioshiriki katika uzinduzi huo huku wengine wakianza kukata bima mara baada ya uzinduzi,waliwashukuru wadau hao na serikali kwa kuwaletea bima ya mazao hivyo ni mategemeo yao kufikia katika kilimo bora na chenye tija kibiashara
Karibia asilimia 65%-70% ya watanzania wanaishi vijijini na wengi wao wanajishughulisha moja kwa moja na shughuli za kilimo za mazao mbali mbali.Shughuli hizi za kilimo zinachangia karibia asilimia 32% ya pato la Taifa kutokana na biashara ya mazao zinazofanyika ndani na nje ya nchi,huku kiasi kikubwa pia cha chakula kinatumika kama chakula kwa jamii kubwa ya waTanzania waishio mijini na vijijini.
Mabadiliko ya hali ya hewa,kuongezeka kwa wagonjwa ya mimea na wadudu, ni baadhi matatizo yanayowakabili wakulima wengi nchini.Matatizo haya yamepelekea wakulima wengi kuacha kujishughurisha na shughuri zingine zisizohisana na kilimo.
Hivyo kampuni ya bima ya Reliance,kwa kushirikiana na na kampuni ya ACRE Africa wataalamu wa kutengeneza bima za mazao Africa,wameanzisha bima hiyo ya mazao kwa wakulima wa mahindi na mpunga Tanzania.Bima hii ya mazao itaanza kupatikana kwa wakulima wa kanda ya kusini katika mikoa ya Njombe,Ruvuma na Morogoro kuanzia msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020.
Lakini ili kuhakikisha wakulima wananufaika na huduma hiyo ya bima,kampuni ya Reliance inashirikiana na taasisi za Alliance for Green Revolution in Africa (AGRA) na Tanzania Association of Professional business Development (TAPDBS) kuhakikisha wakulima wanapata mafunzo ya kutosha kuhusu kilimo bora ili waweze kulima kulima kilimo cha kisasa na na kulinda uwekezaji wao katika kilimo.
Wednesday, November 20, 2019
Bima ya mazao yawifikia wakulima nchini
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





No comments:
Post a Comment