Benki ya Exim Tanzania imetangaza kufungua kituo cha huduma za benki hiyo (Commercial Representative Office) katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.
Hayo yamesema na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt Bernard Kibesse wakati akifungua rasmi tawi jipya la benki ya Exim Tanzania lililopo katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es salaam, baada ya benki hiyo kukamilisha taratibu za umiliki wa iliyokuwa Benki ya UBL Tanzania.
Kufuatia hatua hiyo Benki hiyo inakuwa taasisi ya kwanza ya kifedha nchini Tanzania kuendesha shughuli zake kwenye mtandao wa mataifa matano ikiwemo Ethiopia ambayo inatajwa kuwa ndio nchi ya pili kwa ukubwa wa idadi ya watu barani Afrika.
Mataifa mengine ambayo benki hiyo inaendesha huduma zake ni pamoja Uganda, Comoros na Djibouti.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo jijini Dar es salaam mapema leo ilisema kwamba benki hiyo imepata leseni ya kufungua na kuwa na Ofisi ya Mwakilishi wake nchini Ethiopia kupitia tawi lake la nchini Djibouti na imepanga kuanza kazi kutoa huduma zake nchini humo hivi karibuni.
"Tunatarajia kwamba huduma zetu zitaanza kutolewa kikamilifu mapema mwezi Disemba, 2019 kupitia Ofisi ya Mwakilishi wetu kibiashara iliyopo katika Jengo la Zouleka LKG, ghorofa ya 2, Sub City Bole, 2160 / B. Addis Ababa. '' alisema Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo.
Monday, November 25, 2019
Benki ya Exim Tanzania yaingia Ethiopia
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment