Na Thabit Madai,Zanzibar.
Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalenzo Zitto Zuberi Kabwe amewataka wanachama wake kuonesha Demokrasia ndani ya chama hicho kwa kufanya chaguzi za kuwachagua viongozi kuanzia ngazi za shina hadi Mkoa.
Kauli hiyo aliitoa katika ofisi ya Chama hicho iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar,wakati akitoa tarifa ya kuanza kwa chaguzi hizo za chama ndani ya chama zinazotarajiwa kuanza ctoba 12 mwaka huu.
Zitto alisema ni lazma Demokrasia iliyoota mizizi ionekane namna inavyotekelezwa ndani ya chama hicho.
“Ni lazma tuonyeshe ni namna gani demokrasia imeota mizizi na namna gani demokrasia inavyotekelezwa ndani ya chama chetu “alisema Zitto.
Wakati akitoa tarifa hiyo alisema chaguzi hizo zitafanyika katika Mikoa mitano yenye majimbo 54 ya Zanzibar.ikiwa ni 18 ya Kisiwani Pemba na 34 ya kisiwa cha Unguja, Wodi 111 na Matawi 679.
Hata hivyo alitoa wito kwa wanachama kushirikiana kikamilifu katika ngazi zote za chama kwani viongozi watakaochaguliwa ndio watakaopambana katika chaguzi zijazo.
“Ni wajibu wa mwanachama kuchagua viongozi mahiri,wadilifu watakaohakikisha wanajenga mshikamano mzuri ndani ya chama utakaorahisisha ushindi katika uchaguzi mkuu”alisema Zito.
Aidha amewataka wagombe wote kuomba kura kwa njia ya kidemokrasia na kuepuka ulaghai,ufisadi katika mchakato wa uchaguzi ili baadae kuwa timu moja kwa wagombea wote aliyeshindwa na aliyeshinda.
“wote kwa pamoja watakuwa na wajibu wa kupambana na CCM kwani ni dhahir chama cha ACT ni chama kikubwa cha siasa Tanzania”alisema Zitto.
Hivyo amewasihi kufanya kampeni kwa uhuru na uwazi kwani hakuna kiongozi ambae ameandaliwa kuwa kiongozi kila mwanachama ana haki sawa ya kugombea nafasi hizo.
Aidha ametaka wanachama kuondosha wasi wasi na wahakikishe wanafuata kanuni na sheria za chama, amabapo kamati za rufaa zimewekwa kwa kila ngazi kwa yule asiyeridhika atakuwa na
Friday, October 11, 2019
Zitto awataka wanachama wa ACT Wazalendo kuonesha Demokrasia ya kweli
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment