Adbox

Friday, October 18, 2019

Wanafunzi 30,675 wapewa mikopo

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya shilingi 113.5 bilioni.

Katika mwaka huu wa masomo, Serikali imetenga kiasi cha shilingi 450 bilioni zinazolenga kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, zaidi ya wanafunzi 45,000 ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wenye mikopo wanaoendelea na masomo.

Mwaka 2018/2019, fedha zilizotengwa na kutolewa zilikuwa shilingi 427.5 bilioni na ziliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,283 wakiwemo 41,285 wa mwaka wa kwanza.

No comments:

Post a Comment

Adbox