Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameziandikia barua nchi wanachama zinazodaiwa.
Tatizo kubwa linalosababisha hali hiyo ni upungufu wa kati ya Dola Milioni 200 hadi 250 ambapo wanachama waliolipa michango yao ni 181 kati ya 193.
Inasemekana kuwa Guterres tayari amezikumbusha nchi wanachama kujitoa na kushughulikia hali ya ukata inayopitia UN na wafanye hima katika kulipa madeni yao kuunusuru Umoja huo kwani hadi sasa wamekusanya Asilimia 70 pekee ya michango yote.
Ukata huo umeufanya Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kutumia akiba yake yote na hivyo kuwa na hofu ya baadhi ya shughuli kutofanyika kwa sasa.
Taarifa za makusanyo ya UN zinaonesha kuwa nchi wanachama Saba ambazo ni Marekani, Argentina, Venezuela, Brazil, Mexico, Iran na Israel ndiyo wadaiwa sugu wanaodaiwa Asilimia 97 ya michango.


No comments:
Post a Comment