Adbox

Friday, October 25, 2019

Tsh. Milioni 800 zatengwa kwaajili ujenzi wa daraja la Mbwemkuru

Na Ahmad Mmow-Lindi.

Imeelezwa kwamba jumla ya Tsh. Milioni 800 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa daraja la mto Mbwemkuru itakayo ziunganisha wilaya za Ruangwa na Liwale.

Hayo yalielezwa jana na meneja wa wakala wa barabara za vijijini(TARURA) wa wilaya ya Ruangwa mhandisi, Mashaka Nalupi wakati wa kikao cha bodi ya barabara. Kikao  kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi.

 Mhandisi Nalupi alisema mwaka wa fedha wa 2019/2020 mradi huo umetengewa shilingi 800.00 milioni kwa ajili ya kuanza ujenzi.

 Alisema  taratibu za manunuzi kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma zinaendelea. Ambapo mkataba kwaajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi huo unatarajiwa kuwa tayari ifikapo mwezi Desemba mwaka huu(2019).

Mhandisi Nalupi alieleza kwamba katika kipindi cha Julai 2019 hadi Oktoba 2019 TARURA katika halmashauri ya wilaya ya Ruangwa imepokea shilingi 262,638,637/69 ( 262.63) ikiwa ni kwa ajili ya matengenezo, usanifu, kodi ya jengo la ofisi na miradi ya maendelo. Ikiwawo daraja hilo na lami.

Mbali na hilo la ujenzi wa daraja la mto Mbwemkuru, mhandisi Nalupi alisema TARURA kwa kushirikiana na kampuni ya URANEX imekamilisha makisio ya ujenzi wa barabara za kata ya Chunyu zinazoingia katika eneo la mgodi la Nachu SML.

Akiweka wazi kwamba shilingi 428,703,450.00 zinatarajiwa kutumika kutekeleza mradi huo.

''Kampuni ya TNR Tanzania inafanya upembuzi yakinifu wa barabara ya Ruangwa kwenda Nangurugai yenye urefu wa kilometa 25 kwa ajili ya utanuzi kwa kiwango cha changarawe kuelea katika mgodi wa graphite (bunyu). Mgodi ambao upo katika kijiji cha Nangurugai  kwa makubaliano baina ya kampuni ya TNR na wamiliki wa mgodi, ambao ni kampuni ya LINDI JUMBO LTD,'' alisema Nal.

Hata hivyo, pamoja na mipango hiyo mizuri na yenye faida kwa wananchi, mhandisi  Nalupi baadhi ya  changamoto kwakusema '' Zipo changamoto chache zinazotukabili katika kutekeleza majukumu na wajibu wetu kwa ufanisi.

 Ambazo ni kukosekana fundi sanifu wa barabara, uchakavu wa gari la usimamizi, kutokuwepo jengo la ofisi za TARURA na samani za ofisi  na bajeti kutokidhi mahitaji halisi wa mtandao wa barabara ambao ni kilometa 548.60,'' alisema Nalupi. 

No comments:

Post a Comment

Adbox