Adbox

Saturday, October 26, 2019

TGNP yawapa wanawake mbinu za kushinda uchaguzi

Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Gender Networking Programme (TGNP), limetoa mafunzo ya mbinu mbalimbali za kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wanawake 64 wilayani Songwe mkoani Ruvuma kwa wenye nia ya kugombea kwa lengo la kuwajengea uwezo.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Henry Kigodi, amesema TGNP imejikita katika kusaidia wanawake ambao wana nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuweka usawa kwa kupata viongozi wanawake ambao kwa kipindi kirefu wameshindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kukosa mbinu za kampeni na kukabiliana na mfumo dume.

Kigodi amesema wanawake wakipata uongozi huwa makini katika kufanya maamuzi, kutekeleza na kusimamia shughuli za kimaendeleo kwa kuwa wanawake hukabiliwa zaidi na changamoto za kimaendeleo katika vitongoji, vijiji na mitaani kuliko wanaume.

"Wanawake ni watu pekee wanaohangaika na changamoto zilizopo mitaani kama vile uhaba wa maji, huduma za afya pamoja na malezi napia ni watu wenye ushiriki wa kiwango cha juu katika shughuli za uzalishaji mali kama kilimo lakini hawafaidiki na chochote,” Amesema Kigodi.

Naye mwezeshaji mwenza, Gratiana Rwakibarila, amesema wanawake wanapaswa kutambua kuwa wana uwezo mkubwa katika suala la uongozi, hivyo wanawajibu mkubwa katika kuhakikisha wanapata mbinu za ushindi kwa kupata mafunzo ili kujenga uwelewa.

Aidha, Rwakibarila amesema mafunzo hayo yatawaboreshea mbinu walizokuwa nazo za kampeni wakati wa uchaguzi, Pia ametaja vyama vinavoshiriki mafunzo hayo kuwa ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP pamoja na ADATADEA.

No comments:

Post a Comment

Adbox