Adbox

Saturday, October 26, 2019

TASAF yazipa kaya masikini mamilioni

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini (TASAF) umetoa Dola za Marekani milioni 376.9 ikiwa ni ruzuku kwa kaya masikini milioni 1.1.

Aidha, wanufaika kupitia walengwa wa kaya hizo wanafikia milioni 5.2 na kwa mkoa wa Pwani wamepata walengwa 29,688 na wametoa Sh bilioni 29.9 kwa kaya masikini na zimewezeshwa kupitia ruzuku hizo ambazo hutolewa kwa ajili ya kujikimu.

Akizungumza mjini Kibaha wakati wa kufunga maonesho ya viwanda na biashara ya mkoa wa Pwani, Meneja wa Kuweka Akiba na Kuwekeza kutoka Tasaf, Tatu Mwaruka alisema walengwa hao wamelipwa mara 31.

"Hata Tasaf nayo iko njiani kutekeleza Tanzania ya viwanda. Tunaishukuru serikali kwani walengwa nao wameanzisha viwanda vyao na wameshiriki kwenye maonyesho haya na kuonyesha bidhaa zao ambazo wanazalisha wenyewe," alisema.

Mwaruka alisema kuwa shughuli wanazofanya ni kupata walengwa ambao ni kaya masikini sana na kutoa ruzuku ya fedha kwa ajili ya kujikimu kimaisha na lengo la kutoa fedha hizo ilikuwa ni kusaidia rasilimali watu kwenye kaya ambazo watoto hawawezi kwenda shule na watoto ambao hawaezi kwenda kliniki kutokana na ugumu wa maisha wa hizo kaya “Katika asilimia 38 ya kaya hizo, watoto wameweza kwenda shule na asilimia 16.1 wameweza kuwapeleka watoto kliniki. Tumeweza kuokoa rasilimali watu kwani kama zingebaki hivyo kungekuwa na madhara makubwa ndani ya jamii," alisema Mwaruka.

Alisema TASAF imeanza michakato mbalimbali baada ya kupata fedha hizo za ruzuku, mmojawapo unaoonesha nia ya kuelekea Tanzania ya viwanda ni walengwa kuzalisha bidhaa kama vile sabuni, nguo, mikoba na viatu

No comments:

Post a Comment

Adbox