Adbox

Wednesday, October 16, 2019

TANESCO yaanza ujenzi Ofisi Chato na Geita

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kupitia Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, limeweka jiwe la msingi ujenzi wa majengo ya Ofisi za TANESCO Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi huo chini ya mkandarasi TBA.

Huu ni mwendelezo wa jitihada za TANESCO kuboresha sekta ya huduma kwa wateja na kujenga majengo yake binafsi katika ofisi zote za mikoa na Wilaya Nchini.

Hatua ambayo itasaidia kuondokana na adha ya kupanga nyumba za watu binafsi zenye nafasi ndogo na gharama kubwa.

No comments:

Post a Comment

Adbox