Adbox

Sunday, October 20, 2019

Serikali na Barrick waunda kampuni mpya ya Madini

Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi ametangaza leo kuwa serikali kwa kushirikiana na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni ya ubia inayoitwa Twiga Mineral Corporation.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam Waziri  Kabudi amesema ‘sasa amezaliwa mtoto mpya baada ya Barrick kukubali kumuua mtoto wake, Acacia.’

Kwa mujibu wa Prof. Kabudi akizungumza na waandishi wa habari, katika kampuni hiyo serikali ina hisa asilimia 16 na Barrick asilimia 84.

“Twiga Minerals Company Limited itakuwa na makao makuu yake jijini Mwanza. Kampuni hii imeundwa baada ya kufutwa kwa Acacia iliyokuwa na makao makuu yake jijini London,” alisema Kabudi.

No comments:

Post a Comment

Adbox