Adbox

Friday, October 25, 2019

Sasa mtambue mmechokoza mataifa makubwa - Jaji Warioba

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Warioba amewatahadharisha viongozi wa Afrika waliamua kuamka na kupinga uwekewaji vikwazo kutambua kuwa wamechokoza mataifa makubwa.

Ameeleza kuwa mataifa ndiyo wenye mtindo wa kuweka vikwazo ikiwa ni mbinu za mataifa hayo kushinikiza kukubaliwa kwa matakwa yao.

Amewataka viongozi hao kuwa na msimamo wa kupigana dhidi ya ukoloni 'Mamboleo' kama walivyopambana wakati wa kupigania uhuru na kuwataka kupeleka masuala hayo katika vikao vya Umoja wa Afrika na vikao vingine muhimu ili libebwe kama ajenda kwaajili ya kunusuru mengi yanayoumiza hususan nchi nyingi zinazoendelea.

Pia Jaji Warioba ameitaka SADC na nchi za Afrika kupiga kelele kuhusu kuwekewa vikwazo kwa baadhi ya nchi na kuongeza kuwa licha kutaka vikwazo kuondolewa nchini Zimbabwe lakini pia suala la mgogoro wa ardhi kwa Zimbabwe na Afrika Kusini nalo litafutiwe suluhu.

No comments:

Post a Comment

Adbox