Adbox

Saturday, October 19, 2019

Rais wa Andres Manuel Lopez Obrador atetea mtoto wa El Chapo kuachiliwa

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador, ametetea uamuzi wa kumuachilia huru mtoto wa mlanguzi wa kimataifa wa dawa za kulevya Joaquin "El Chapo" Guzman, aitwaye Ovidio Guzman.

 Ovidio aliachiliwa baada ya vikosi vya usalama kuzidiwa nguvu na wafuasi wa mtandao wa El Chapo.

Rais Obrador amesema anatambua kuwa hali ilikuwa ngumu wakati polisi walipokabiliana kwa risasi na kundi hilo Alhamisi. Amesema, kukamatwa kwa mhalifu mmoja hakuna thamani zaidi ya maisha ya raia.

Awali, mkuu wa vikosi vya usalama Alfonso Durazo alisema maafisa wa jeshi la ulinzi walikuwa wakilinda doria kwenye eneo la Culiacan walipoanza kushambuliwa kutoka nyumba jirani.

Maafisa hao walijibu mashambulizi na kuwakamata watu wanne, akiwemo mtu aliyejitambulisha kama Ovidio Guzman Lopez.

Ovidio alishtakiwa nchini Marekani mnamo mwaka 2018 kwa kusambaza dawa za kulevya. Mahakama ya Marekani ilimhukumu baba yake Joaquin "El Chapo" Guzman kifungo cha maisha jela.

No comments:

Post a Comment

Adbox