Adbox

Saturday, October 12, 2019

Rais Magufuli atoa neno kwa viongozi watakaoshindwa kuhamasisha uandikishaji Serikali za mitaa

Rais Magufuli amewataka viongozi wa mikoa kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.

 “Jana Waziri alitoa takwimu za baadhi ya mikoa iliyofanya vizuri. Ninafuatilia lakini alitoa baadhi ya mikoa inayoendelea kufanya vibaya. Zoezi likikamilika nitataka Waziri anipe taarifa za mikoa iliyofanya vizuri na iliyofanya vibaya.”

“Nataka niseme hapa hadharani, ile mikoa ambayo watu wao watashindwa kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura nitawashangaa. Ninajua Watanzania hawatanilaumu kwa hatua zitakazochukua,” amesema Magufuli.

Ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo kuahidi kupeleka pendekezo maalum kwa mikoa itakayofanya vibaya katika uandikishaji wakati akitoa taarifa za zoezi hilo jana mkoani Katavi mbele ya kiongozi mkuu huyo wa nchi.

No comments:

Post a Comment

Adbox