Adbox

Tuesday, October 15, 2019

Rais Magufuli aagiza waliojilipa mamilioni Lindi kurudisha

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka watendaji wa serikali waliojilipa fedha kiasi cha Sh. 49 milioni zilizokuwa za ukarabati wa wodi ya watoto katika hospitali ya mkoa ya Sokoine mkoani Lindi kuzirudisha mara moja.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo  wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiwalala jimbo la Mtama wakati akienda Wilaya ya Ruangwa kwa ziara.

“Matumizi mabaya ya fedha za ukarabati wodi ya watoto, mfano watendaji kutumia Sh49 milioni kujilipa na wako hapa hapa.”

“Nataka watendaji wote waliojilipa hizo fedha wazirudishe, nimeona niyazungumze haya mapema ili hospitali ya wilaya Mtama watendaji wasije wakaenda kujilipa, fedha yote Sh1.5 bilioni ni kwa ajili ya kujenga hospitali,” amesema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Adbox