Adbox

Friday, October 25, 2019

Nchi za SADC kuendeleza mikakati ya Itifaki za pamoja kukuza maendeleo ya Sekta za mazingira , Maliasili na Utalii

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangalla mikutano yote ya wataalamu na maktibu wakuu wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika ililenga kujadili na kutoa mapendekezo ya juu ya masuala mbali mbali yanahusu sekta za mazingira maliasili na utali kwa lengo la kuhakikisha zinaendelea kuchangia maendeleo ya sekta hiyo kwenye ukanda huo wa SADC.

Dkt.Kigwangalla ameyasema hayo wakati akimkaribisha makamu wa Raisi Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano wa pamoja wa mawaziri wanaosimamia  sekta za Mazingira maliasili na Utalii kwa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC unaoendelea jijini hapa.

Alisema kuwa jukumu la mkutano huo wa ngazi ya mawaziri ni kuridhia mapendekezo yaliowasilishwa na wataalamu ambayo yanalinda maslahi ya jumuiya katika mkutano huo majadiliano yetu yatajikita katika kupima utekelezaji wa sera na mikakati mbalimbali ikiwemo itifaki mbali mbali.

Akazitaja baadhi ya itifaki hizo kuwa ni pamoja na itifaki ya SADC ya uhifadhi wa wanyamapori pamoja na mikakati ya utekelezaji wa hima sharia na mipango ya kupambana na ujangili na mpango wa SADC ya maeneo ya uhifadhi yanayovuka mipaka.

Ameendelea kueleza itifaki hizo ni pamoja na itifaki ya SADC kuhusu usimamizi wa misitu na mkakati wa mistu ikiwemo pia itifaki ya Sadc kuhusu maendeleo ya utalii na mipango ya maendeleo ya utalii, ikiwemo pia itifaki ya SADC ya usimamizi wa mazingira kwa maendeleo endelevu yenye mkakati wa mabadiliko ya tabianchi yenye mipango ya SADC ya kupambana na uenezaji wa jangwa.

Akatanabaisha kuwa mazingira ya mabadiliko ya tabianchi yanachangai kuathiri kwa kiasi kikubwa uchimi wa mataifa hayo yanaotegemea uwepo wa sekta ya utalii kupata kuongeza fedha katika kukuza uchumi wan chi hizo hivyo wanakutana kujadili kwa kina kuona ni namna gani wataweza kupambana na hali hiyo kwa kina ilikuondoa changamoto zinazoikabili nchi za ukanda huo.

Kwa upande wake Waziri wa habari utamaduni na mambo ya kale Mahmoud Thabit Kombo alisema kuwa Zanzibar teyari imekuwa kwenye mipango hiyo ya kuhakikisha masuala ya mazingira ya bahari na machafuko ya viumbe wanaendeleo kuthibiti kwa ajili ya sasa na kizazi kijacho.

Alisema kuwa Zanzibar imekuwa ikitegemea kuendesha uchumi wake kwa kutegemea sekta hiyo na kutoa mfano kuwa mwaka 2018  watalii zaidi ya 550,000 waliitembelea huko na kuwataka kuwashirikisha wananchi kuhakikisha wanaendelea kutunza mazingira kama mipango ya serikali kwenye kuelekea uchumi wa Blue.

Akatanabaisha kuwa Mh.Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Dkt.Ally Mohammed Shein Alimwakilisha mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Mgafuli kwenye mkutano wa masuala ya uchumi wa Bahari na machafuko ya viumbe waishio humo hii ni kusisitiza na kuonyesha jinsi nchi yetu imejikitaka kuhakikisha inaendelea kutunza mazingira na kuheshimu itifaki zake.

‘’Maendeleo endelevu katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar yameelekezwa kwenye kuhakikisha utunzaji wa Rasilimali kukuza utalii na utunzaji wa mazingira kwa ajili ya kuendeleza utalii kwa faida ya wazanzibar’’ asisitiza Thabiti Kombo

No comments:

Post a Comment

Adbox