Adbox

Thursday, October 17, 2019

Madinah: Mahujaji 35 wafariki katika ajali ya basi

Mahujaji 35 wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali ya basi karibu na mji mtakatifu wa Saudia wa Madinah.

Ajali hiyo ilitokea Jumatano jioni wakati basi lililokuwa limebeba mahujaji 39 wa nchi tofauti za Asia na Kiarabu lilipogongana na gari lingine katika Kituo cha Al-Akhal eneo la Madinah.

Polisi wa Madinah wameanzisha uchunguzi ili kubaini kilichosababisha ajali hiyo.

Gavana wa Madinah Prince Faisal bin Salman bin Abdulaziz alituma ujumbe wa rambirambi kwa jamaa na marafiki wa waathirika na kuwatakia afueni ya haraka kwa waliojeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

Adbox