Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Polledo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es salaam hapo jana.
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, pamoja na mambo mengine, amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendeleza ushirikiano wa kihistoria na kindugu na Chama Cha Kikomunisti cha Cuba.
Aidha, Katibu Mkuu akipokea salamu hizo kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemuhakikishia Balozi huyo kuwa, CCM itaendelea kufuata nyayo za Waasisi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Fidel Castro ambao wamevijenga vyama hivi katika misingi ya Undugu, Ushirikiano na Mshikamano.
Thursday, October 17, 2019
Katibu Mkuu wa CCM afanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment