Adbox

Monday, October 21, 2019

Kamati yaandaliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli

Adelina Kapaya-Katavi

Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa  wa Katavi, John Lomuri ameunda kamati maalumu ya kushughurikia maandalizi ya kuhamisha ofisi  zote za  Wilaya ya Tanganyika kutoka katia wilaya ya Mpanda kuhamia ndani ya wilaya ya Tanganyika.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri  ya Mpanda, Samson Medda na kubainisha kuwa wako kwenye mkakati wa kuhakikisha wanahamia katika Halmashauri ya Tanganyika kutokana na agizo la Rais  na ifikapo wiki ijayo Ofisi ya Mkurugenzi  itahamia katika jengo  la Hospitali ya Wilaya  huku ujenzi ukiendelea.

Samson ameongezea kwa kusema kuwa licha ya ofisi zao kuwa mbali na Wilaya yao wamekua wakifanya kazi zao kwa uadilifu  kwa kuwahudumia wananchi  pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili  kwa muda  mwafaka na kuyatafutia suluhu

 Licha ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Magufuli kutoa agizo  kwa wakurugenzi  wote nchi nzima kuhakikisha wanahamia katika wilaya zao, wilaya ya Tanganyika ilikuwa imeshaanda maeneo ya kujenga ofisi za Halmashauri kwa lengo la kuihudumia jamii kwa ukaribu zaidi ili kupunguza gharama za usafiri wakati wa utendaji

Mnamo  October 7 mwaka huu Rais Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mtendaji  wilaya ya Tanganyika  kuhakikisha wanahamia katika Halmashauri yao na ofisi zao zote ziwe ndani ya wilaya husika kwa muda wa siku 30.

No comments:

Post a Comment

Adbox