Adbox

Tuesday, October 29, 2019

CCM yawaonya wanaotumia rushwa kusaka uongozi

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula amesema kuwa, chama hicho hakitamvumilia Mwanachama yeyote anayetumia rushwa kutafuta uongozi.

Mangula ametoa kauli hiyo mkoani Simiyu wakati wa kikao cha utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani humo.

 "Hatutaki viongozi wapenda rushwa, tunataka watu wenye moyo wa kuwatumikia Wananchi, maana rushwa ni adui wa haki, yeyote atakayetumia fedha zake kununua kura hata kama atapata kura nyingi kiasi gani tutamfyekelea mbali," amesisitiza Mangula.

No comments:

Post a Comment

Adbox