Adbox

Monday, September 30, 2019

Waziri Mkuu kufungua Maonyesho ya Sido mkoani Singida

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kufanya Ziara ya siku nne  ya Kikazi Mkoani Singida, kwaajili ya kukagua  na kutembelea miradi ya Maendeleo ikiwemo ile mikubwa ya Kitaifa  na kufungua rasmi maonyesho  ya SIDO Kitaifa mjini Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Ofisini kwake  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi amesema ziara ya waziri itaanzia katika Wilaya ya Manyoni akitokea Mkoani Dodoma na kuhitimisha siku ya Jumatatu ya October 8 mwaka huu.

Naye Mkurugenzi mkuu wa SIDO Profesa Sylvester Mpandu amesema kuwa maonyesho ya mwaka huu yatakuwa na mvuto mkubwa kutokana na ushiriki wa  mataifa Makubwa ikiwemo China,India na Afrika kusini ambayo  yamepiga hatua kubwa kwa teknolojia ya Viwanda.

No comments:

Post a Comment

Adbox