Na Thabit Madai,Zanzibar
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamasha la Pili la Urithi wa Utamaduni wa Mtanzania katika ukumbi wa Ngome Kongwe , Forodhani Mjini Unguja.
Alitoa tarifa kwa Waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale, Chum Kombo Khamis amesema kuwa tamasha la urithi wa utamaduni ni la pili la utamaduni wa Mtanzania.
Aidha alisema kuwa tamasha la urithi mara hii litasherehekewa katika mikoa 12 ambayo kila mikoa imepewa nafasi ya kuibua na kuitangaza zao maalum la utalii ikiwemo hifadhi za taifa ,utamaduni pamoja na Tamasha la utalii la Zanzibar.
Alisema kuwa lengo la tamasha la urithi ni kuendeleza pamoja na kuimarisha na kutangaza alama na tunu za taifa ili kudumisha umoja na uzalendo wa taifa.
Vilevile Naibu Chum alisema kuwa tamasha hilo pia litaweza kuhamasisha ,kutambua,kuhifadhi na kudumisha mila ,lugha na desturi za mtanzania kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Hata hivyo alisema kuwa katika tamasha hilo la urithi mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo burudani za ngoma za asili pamoja na michezo mbalimbali .
Aidha alisema kuwa tamasha hilo pia litaweza kusaidia kuongeza siku za ukaazi kwa watalii na kupelekea taifa kupata mapato zaidi yanayotokana na watalii.
Thursday, September 26, 2019
Waziri Kigwangala kuwa mgeni rasmi tamasha la Mtanzania
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment