Na Amiri kilagalila, Njombe
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ametoa siku ishirini kwa mkandarasi na injinia kuhakikisha umeme unafikishwa katika kijiji chote cha Lole kilichopo lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe.
Waziri Kalemani ametoa agizo hilo kijijini hapo wakati akiwasha umeme uliofikishwa katika kanisa la Tanzania assembles of God T.A.G.
“Ndugu zangu hapa kazi bado,mkandarasi na Injinia nataka kijiji cha Lole chote na vitongoji vyake vyote saba vipatiwe umeme,na hii kazi ianze mara moja kuanzia kesho,kwanza kijiji wala sio kikubwa sana, wananchi 40 wamelipia na mmewapa umeme, sawa wako wananchi zaidi ya mia mbili bado, nataka vitongoji vyote ndani ya siku 20 vipelekewe umeme vyote,”alisema Kalemani.
Aidha waziri kalemani ametoa wito kwa wananchi kuendelea kulipia kiasi cha shilingi elfu 27 na sio kufuatilia nguzo kwa kuwa hilo sio jukumu la mwananchi.
Katika hatua nyingine waziri Kalemani amemtaka meneja wa Tanesco mkoa wa Njombe kuhakikisha anawakabidhi wananchi vifaa vya umeme wa UMETA 250 vilivyopo katika mradi ndani ya jimbo la Lupembe kuepuka ghalama ya waya.
“Kama una nyumba yako ina vyumba viwili na sebule au vitatu na sebule usihangaike ghalama ya nyaya tumia chombo hiki,tena kwenye mradi vipo 250 vya bure,kwa hiyo wakandarasi muwapatie wananchi vyombo hivi”aliongeza Kalemani
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Joramu Hongoli ameishukuru serikali kwa kuwa jimbo la Lupembe mpaka sasa ni kata mbili pekee ambazo bado hazijafikiwa na umeme.
“Ninakushukuru sana Waziri na serikali,mpaka sasa vijiji vilivyokosa umeme vimeendelea kupunguzwa na kwa hiyo mpaka sasa kwa leo ni kata mbili peke yake za Mfiliga na Ilamba umeme haujaanza kunusa,”alisema Hongoli
Baadhi ya wananchi wa kata ya Ikuna na Ninga akiwemo Petro Malekela wamesema kuzinduliwa kwa umeme katika kata zao kutasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma mbali mbali ikiwemo utoaji wa kopi.
Waziri kalemani amewasha umeme katika kanisa la T.A.G lililopo katika kijiji cha ikuna pamoja na kituo cha afya ninga kilichopo kata ya Ninga jimbo la Lupembe wilayani Njombe mkoani humo.
Monday, September 2, 2019
Waziri Kalemani atoa siku 20 kwa kijiji hiki kufikishiwa Umeme
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment