Adbox

Friday, September 27, 2019

Wakuu wa Mikoa,Wilaya watakiwa kuendelea kupunguza vizuizi kwa wakulima

Na Ahmad Mmow, Lindi

Wakuu wa Wilaya na Mikoa nchini wameaswa waendelee kupunguza utitiri wa vizuizi vya barabarani ili kuwasaidia wakulima kufikisha mazao sokoni.

Wito huo ulitolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa wakati wa mkutano wa mashauriano baina ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara waliopo katika mkoa wa Lindi, ambao ulifanyika katika manispaa ya Lindi.

Waziri Bashungwa alisema Halmashauri nyigi zinavizuizi vingi, hali inayosababisha mazao kushindwa kufikishwa sokoni kwa wakati. Kwahiyo kunahaja ya wakuu wa mikoa na wilaya kuendelea kupunguza vizuizi hivyo ambavyo vinasababisha ugumu wa  kusafirisha mazao mbalimbali. Yakiwemo mazao ya kilimo.

Alisema halmashauri zisiwe miongoni mwa sababu zinazokwamisha bidhaa kufikishwa sokoni. Badala yake ziwe msaada , kwani bidhaa hizo zikifikishwa sokoni na kuuzwa zitachangia kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Alisema vizuizi vimekuwa vingi kiasi cha kuwa kama mipaka ndani ya nchi. Kwahiyo kunahaja ya kupunguza vizuizi hivyo ambavyo vimegeuka kuwa kero kwa wasafirishaji bidhaa na mazao.

Mbali na hilo la vizuizi, Bashungwa alisema katika muda wa miezi mitatu aliyohudumu katika wizara hiyo amejifunza mengi  kuhusu korosho. Akiweka wazi kwamba zinaweza kubadilisha  maisha ya wakulima. Kwahiyo hafurahishwi kuona wananunuzi wa zao hilo wanashindwa kupata kiasi wanachohitaji kutokana na uzalishaji mdogo.

"Wafanyabiashara wanaomba kiasi kikubwa, lakini kwakuwa uzalishaji ni mdogo zinakuwa zimekwisha. Kwahiyo kunahaja ya kuongeza uzalishaji," alisema Bashungwa.


Kutokana na ukweli huo, waziri huyo mwenye dhamana ya viwanda na biashara alisema serikali inamikakati kabambe ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo linalimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

No comments:

Post a Comment

Adbox