Adbox

Tuesday, September 3, 2019

Wafuasi wa mgombea urais aliyeko jela waandamana

Wafuasi wa mgombea urais aliyefungwa jela nchini Tunisia Nabil Karoui wanaandamana kudai aachiliwe huru ili aweze kufanya kampeini yake kwa uhuru kuelekea uchaguzi utakaofanyika Septemba 15.

Majaji wanajiandaa kutoa uamuzi leo Jumanne kuhusu ssuala hilo la ama kuachiwa huru mwanasiasa huyo na kusubiri uchunguzi zaidi ufanyike kuhusu tuhuma za kuhusishwa kwake na utakatishaji fedha pamoja na kukwepa kodi.

Wafuasi chungunzima wa Karoui walikusanyika nje ya mahakama ya Tunis ambako kunafanyika kikao cha faragha kinachojadili uamuzi wa kutolewa, wakipaza sauti za kudai aachiliwe huru.

 Wafuasi wa mwanasiasa huyo wanasema tuhuma zinamuandama Karoui zimechochewa kisiasa kwasababu alikamatwa muda mfupi kuelekea uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Adbox