Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile amesema wana mpango wa kuhamishia kambi ya upimaji virusi vya ukimwi kwenye viwanja vya michezo ili kuhamasisha wanaume kujitokeza kupima.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea maonesho ya Utamaduni ya Jamafest, Dk Ndungulile alisema sababu kubwa ya kutaka kuhamishia kambi viwanjani ni baada ya kugundua wanaume wengi wanakwepa kupima, huku baadhi yao wakionekana kufa zaidi kwa kutozingatia maelekezo.
"Wanawake wengi wamekuwa wakijitokeza kuliko wanaume, tumeona twende kwenye makambi kuwafuata na mojawapo ni viwanja vya michezo ili kutoa elimu ya upimaji kwao," alisema.
Alisema hata kwa baadhi wanaokutwa na maambukizi huchelewa kuanza dawa za kuua makali jambo ambalo limechangia baadhi kufa mapema huku akiwahimiza kuuona ugonjwa huo wa kawaida kama yalivyo mengine.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo alisema ujio wake katika tamasha hilo una mahusiano makubwa na Utamaduni kwasababu wamekuwa wakifanya kazi na wasanii mbalimbali kufikisha jumbe za afya.
"Michezo, sanaa na Utamaduni yana mahusiano tumekuwa tukifanya nao kazi, lakini pia ningependa kuona wasanii wanaibua mada mbalimbali za afya kwa mfano masuala ya lishe na mambo mengine tuweze kuyafanyia kazi," alisema.
Friday, September 27, 2019
Upimaji ukimwi kuhamia viwanja vya michezo, kisa?
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment