Adbox

Thursday, September 26, 2019

Serikali kujenga mitambo mipya ya Umeme Mtwara

Katika kuhakikisha kuwa Mkoa wa Mtwara unakuwa na umeme wa uhakika kwa muda wote, Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaeleza wafanyabishara na wawekezaji wa Mkoa huo kuwa, Serikali ipo mbioni kujenga mitambo miwili mipya ya umeme.

Alisema hayo wakati alipokuwa ajibu hoja za wadau wa maendeleo katika  mkutano uliolenga kusikiliza  changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Mtwara, ambapo alisema Serikali inazifahamu changamoto zote za umeme zinazojitokeza katika mkoa huo na tayari zinafanyiwa  kazi.

“Kituo cha umeme cha Mtwara kina zaidi ya miaka 10 na baadhi ya mitambo imechakaa, hapa ninavyozungumza sasa mitambo inayofanyakazi ni ile miwili tu mipya, na mahitaji ya umeme katika mkoa wa Mtwara na Lindi yameongezeka,  kwani kwa sasa inatakiwa takriban megawati 17.7 wakati uwezo wa uzalishaji katika Kituo cha Mtwara ni megawati 18 hivyo tunafanya jitihada za kuongeza mitambo mipya.”Alisema Mgalu.

Alifafanua, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), katika mwaka huu wa fedha imetenga bajeti ya kununua mitambo miwili ambayo itasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Vile vile, Naibu Waziri alisema hatua nyengine ambayo Serikali imechukua ni pamoja kuwa  na mpango wa muda mrefu utakaosaidia utapatikanaji wa umeme wa uhakika mkoani humo.

“Tunatarajia kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi hapa hapa Mtwara wa megawati 300 na njia ya kuusafirisha, pale Somangafungu pia kuna mpango wa kujenga mtambo wa kuzalisha megawati 240 kwa  kutumia gesi  na njia ya kuusafirisha kutoka Somangafungu hadi Kinyerezi, njia zote  zitakuwa na  msongo wa kV 400 na tunategemea  kutekeleza huu mradi kati ya mwaka 21/23.”alisema Mgalu

No comments:

Post a Comment

Adbox