Adbox

Friday, September 27, 2019

Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini

Na Ahmad Mmow, Lindi

Serikali imesema kutokanana kutambua na kuthamini mchango wa   wawekekezaji katika kuchangia ukuaji wa uchumi itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki. Alipozungumza kwenye mkutano wa mashauriano baina ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara waliopo katika mkoa wa Lindi. Ambao ulifanyika katika manispaa ya Lindi.

Waziri Kairuki alisema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara na kushughulikia kutatua kero na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hizo ili kuhakikisha kunakuwepo mazingira bora zaidi kwa uwekezaji na biashara.

Alisema kwa kuzingatia ukweli huo na nia thabiti iliyo njema kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini, inatarajia kupeleka mswada maalumu bungeni kwaajili ya  kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara. Mswaada ambao utakuwa na marekebisho mbalimbali yanayohusu biashara na uwekezaji.

Waziri Kairuki aliendelea kuwatoa hofu wawekezaji kwa kusema kwamba mbali na kupeleka mswada huo bungeni, lakini pia kutakuwa na mabadiliko ya sheria ya uwekezaji. Kwahiyo kabla ya kufika mwaka ujao kutashuhudiwa mabadiliko. Ikiwamo kituo cha uwekezaji( TIC) kuongezwa nguvu ili kiweze kuwa na maamuzi makubwa yenye tija kwa wawekezaji na taifa.

Sanjari na hayo, waziri huyo mwenye dhamana ya uwekezaji alibainisha kwamba serikali itaendelea kufanya mapitio ya sera ya uwekezaji. Kwahiyo wasisite kujisajili kwenye kituo cha uwekezaji, kwani mikakati iliyopo itakuwa na tija kubwa kwao.

Aidha waziri Kairuki alionya kwamba serikali haitasita kumchukulia hatua za kisheria yeyote atayeendelea kutoza kodi zilizofutwa au  mambo yaliyopata msamaha. Akiweka wazi kwamba kuendelea kufanya kilichokatazwa ( kutoza kodi zilizoondolewa) ni kosa.

"Wakuu wa taasisi, hasa watendaji shukeni chini ili muwalee wawekezaji na wafanyabiashara kwa kuwafundisha na kuwasaidia jinsi ya kutatua changamoto zilizopo kwenye shughuli zao," aliagiza Kairuki.


Katika hali inayodhihirisha serikali imeamua kwa dhati kuvutia wawekeji nchini, waziri huyo amezitaka halmashauri nchini zitenge bajeti kwa ajili ya maeneo ya uwekezaji. Kwani zinatakiwa kutenga maeneo  yatayotumika kwa shughuli hiyo.

No comments:

Post a Comment

Adbox