Serikali ya Tanzania imesema ipo katika mchakato wa kufungua kesi ya kudai fidia ya pesa iliyotumika kuendeshea kesi ya Ndege ya ATCL, iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na EATV Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt Damas Ndumbaro, amesema kuwa licha ya wao kushinda kesi dhidi ya kushikiliwa kwa ndege ya ATCL, lakini lazima itachukua hatua stahiki dhidi ya aliyefungua kesi hiyo.
''Sisi tumemaliza kesi kinachofuata ni kudai fidia kwa sababu Mahakama imetupa gharama yote ya kesi, kwahiyo tutadai gharama za kesi na fidia ya hasara ambayo tumeipata kutokana na kesi hii'', amesema Waziri Ndumbaro.
Ndege hiyo aina ya Airbus A220-300 ilizuiliwa nchini Afrika ya Kusini kwenye uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, kwa amri ya Mahakama, siku ya Agosti 24 na iliachiwa huru Septemba 4, 2019, hii ni baada ya Serikali kutuma jopo la Mawakili kwa ajili ya utetezi wa kesi hiyo.
Thursday, September 5, 2019
Serikali kudai fidia ya ndege iliyozuiliwa Afrika Kusini
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment