Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewataka watumishi wa serikali kutokuwa na woga wa kumiliki ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwamo kujenga makazi bora ya kuishi pamoja na uwekezaji wa miradi ya kiuchumi isipokuwa wasivunje sheria ya nchi.
Wito huo ulitolewa wilayani Masasi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri za Wilaya ya Masasi, madiwani, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na watendaji wa taasisi za kiserikali.
Byakanwa alisema kitendo cha kusubiri kustaafu ndipo kuanza kujenga makazi ya kuishi au kufanya uwekezaji wa aina yoyote kwa mtumishi sio sahihi bali uwekezaji lazima mtumishi afanye wakati bado yupo kazini.
Alisema wapo baadhi ya watumishi mkoani humo ambao wamekuwa wakichelewa kufanya shughuli za kiuchumi au kujenga nyumba bora za kuishi kwa kisingizio kuwa wao si wazawa wa eneo wanalofanyia kazi.
Alisema kusubiri kuhamishwa au kustaafu kazi ndipo kufanya shughuli za kimaendeleo ni kuchelewa kujiletea maendeleo kwa mtumishi.
Alisema kila mtumishi ana haki ya kumiliki ardhi kuanzisha miradi ya kimaendeleo ilmradi sheria ya nchi isivunjwe, hivyo watumishi waangalie fursa zilizopo kwenye maeneo yao na kuzitumia katika kujiletea maendeleo.
"Kuna watumishi hawataki kufanya uwekezaji au kujenga nyumba za kuishi kwenye wilaya wanazofanyia kazi eti kwa vile watahamishwa na pia sio wazawa wa maeneo haya hii sio sababu ya msingi tuwekeze sasa kabla ya kustaafu,” alisema Byakanwa.
Alisema watumishi lazima watafakari kwa kina juu ya maisha yao ya baadaye kuanzia sasa wakati wapo kazini kwa kuwekeza vitega uchumi mbalimbali ambavyo pale wakiondoka kazini wasihangaike tena kupigania maisha yao.
Wednesday, September 25, 2019
RC awapa mbinu Watumishi cha kufanya kabla ya kustaafu
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment