Na Timothy Itembe, Mara
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Saimon Sirro amesema kuwa Askari wa jeshi lake wamekamata Boti ya Uganda ikiwa inafanya uvuvi haramu ndani ya Maji ya Ziwa Vikitoria kwenye mipaka ya Tanzania.
Sirro ametumia nafasi hiyo kusema kuwa kitendo hicho kimeibua hisia kubwa na changamoto ndani ya jeshi hilo na Jeshi hilo ili kuchukua hatua ya kufanya mazungumzo ya haraka ya ujirani mwema baina ya Uganda na Tanzania ili kuzuia na kukomesha vitendo hivyo.
Kamanda huyo aliongeza kuwa mchakato wa kuwakutanisha IGP wa pande zote mbili Uganda na Tanzania unatarajia kufanyika hivi karibuni ndani ya mwezi wa Tisa mwaka ya ujirani mwema huku mazunguzo hayo yakishirikisha viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa Jeshi la polisi wa nchi hizo mbili IGP.
"Askari wetu hivi karibuni wamekamata Boti ya Uganda ikiwa inafanya uvuvi haramu ndani ya Ziwa Vikitoria na tumefanya mawasiliano na IGP wa Uganda ili kukutana pamoja na kufanya mazungumzo kwa lengo la kukomesha vitendo haramu vinavyofanywa ndani ya Ziwa vikitoria na maharamia"alisema Sirro.
Pia IGP Sirro amewaambia waandishi wa habari kuwa jeshi lake litahakikisha kuwa Wavuvi ndani ya Ziwa Vikitoria ambao wanafanya shuguli hizo kihalali wanafanya kwa Amani na kwa Usalama bila kubugudhiwa huku wakichangia kukua pato la Taifa.


No comments:
Post a Comment