Wahandisi Vijana wanaohitimu Vyuo Vikuu na Vyuo vya Elimu ya Juu nchini wametakiwa kuunda Kampuni na kuchangamkia fursa mbalimbali za ujenzi zinazotolewa na Halmashauri za Wilaya na Manispaa nchini.
Hayo yamesemwa jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja na Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde wakati wa kufungua maonesho ya ubunifu wa kazi za kihandisi yaliyojumuisha washiriki kutoka Vyuo mbalimbali nchini ambapo ameeleza bayana dhamira ya Serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na BRELA kuwajengea uwezo na uelewa wa masuala ya Biashara kwa kuwafanya kuwa rasmi kupitia vyombo vya uendeshaji biashara ikiwemo makampuni ili kuwapa nafasi kubwa ya kushiriki katika kazi mbalimbali za miradi midogo midogo ya ujenzi kupitia force account.
"Ni dhahiri kwamba hatuwezi kuwa na uchumi wa viwanda madhubuti kama hatutaweka nguvu kubwa katika masuala ya uhandisi,hawa ni pacha.Ofisi ya Waziri Mkuu tutashirikiana na COSTECH pamoja na BRELA kuhakikisha bunifu hizi zinaleta tija kwa maslahi mapana ya Taifa na kukua kwa taaluma zenu.Natamani kuwaona Vijana mnajikusanya kwa kuunganisha nguvu na kuunda makampuni ili mchangamkie fursa mbalimbali za ujenzi wa miradi midogo midogo kama sehemu ya kujiajiri na kuajiri Vijana wengine,"Amesema Mavunde
Naye Msajili wa Bodi ya Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Patrick Balozi ameishukuru Serikali kwa kuwapa ushirikiano mkubwa na kuwawezesha Wahandisi Vijana kimafunzo na pia kwa kuwaunganisha na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa lengo la kukuza tasnia ya Uhandisi nchini na kwamba kama Bodi wataendelea kuwalea na kuwaandaa Vijana hao kuwa wahandisi wazuri na wa kutegemewa nchini kwa kuwapatia nafasi za mafunzo ya vitendo.
Wakati huo huo Naibu Waziri Mavunde ameahidi kuwatafutia ufadhili kupitia makampuni mbalimbali makubwa wabunifu wa mkaa wa makaratasi,machine ya kuchakata nyanya na mbunifu aliyetengeneza fimbo ya watu wenye ulemavu wa macho yenye uwezo wa kumpa ishara ya mlio kama atakuwa anaelekea kwenye kitu kinachoweza kumdhuru.
Sunday, September 22, 2019
Naibu Waziri Mavunde awataka wahandisi vijana kuunda Kampuni
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment