Na Rahel Nyabari, Tabora
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Mzee Mkongea Ally amekataa kuzindua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Chang'a iliyopo Kata ya Tumbi Manispaa ya Tabora baada ya kutilia shaka matumizi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni nne.
Katika mradi huo wananchi wamechangia kiasi cha shilingi milioni kumi, Serikali kuu shilingi milioni ishirini na moja huku Halmashauri katika ripoti hiyo ikionesha kuchangia kiasi cha shilingi milioni tatu wakati uhalisia ikielezwa ni shilingi milioni Saba, wasiwasi ukaibuka katika matumizi ya milioni nne ambayo hayakuonekana kwenye ripoti ya utekelezaji .
Ally ameagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tabora kufanya uchunguzi wa kina na kutoa majibu ndani ya wiki mbili ili kuweza kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakaye husishwa sheli ichukuliwe zidi yake .
Hata hivyo Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru amemtaka mkuu wa wilaya ya Tabora Komanya Erick Kitwala baada ya kufanyika kwa uchunguzi huo kuzindua na kuweka jiwe la msingi kwa niaba ya kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2019.
Monday, September 2, 2019
Mwenge wa Uhuru wakataa mradi wa Madarasa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment