Adbox

Tuesday, September 24, 2019

Mkutano wa UN wakutanisha viongozi wa dunia New York

Viongozi na wakuu wa nchi ulimwenguni wanakutana katika mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kuufungua mkutano huo. Hapo awali watoto 16 ambao ni wanaharakati wa kutetea mazingira waliwasilisha malalamiko yao rasmi kwa Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watoto wakilalamikia namna ambavyo serikali zinavyoshughulikia mabadiliko ya tabia nchi.

Mwanaharakati mwenye umri mdogo Greta Thunberg ambaye amekuwa mstari wa mbele kuzitaka serikali ziwajibike amesema.

Mkutano huo unafanyika wakati mataifa yanakabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi, migogoro ya kikanda na uwezekano wa kutokea mzozo wa Mashariki ya Kati unaoweza kuathiri dunia nzima.

No comments:

Post a Comment

Adbox