Adbox

Monday, September 30, 2019

Mkutano wa Mbowe wazingirwa na Polisi

Mkutano wa ndani wa Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi  ya Upinzani Bungeni umevamiwa na Polisi Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Wakiongozwa na mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Lwelwe Mpina wamevamia mkutano huo leo  kwa maelekezo ya mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Mkuu huyo wa Wilaya amethibitisha kutuma polisi hao akisema amefanya hivyo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa Mbowe na viongozi wengine pamoja na wananchi, akisema hawana sababu ya kutaharuki kama ni raia wema.

"Mkutano wa chama cha siasa sio send off au harusi. Mkutano wa chama cha siasa polisi wana haki ya kuwepo. Hata mikutano ya CCM polisi wanakuwepo," amesema.

Polisi walifika katika ofisi za Chadema wilaya ya Hai na kulazimisha kuingia ndani ya mkutano huo ili kujua nini kinachozungumzwa kwa lengo la kusimamia ulinzi na usalama kwao na kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Adbox