Adbox

Monday, September 2, 2019

Mahakama leo kutoa maamuzi kuhusu ombi la Tundu Lissu kuzuia kuapishwa Mbunge wa CCM

Mahakama kuu masijala ya Dar es salaam leo itatoa maamuzi kuhusu ombi la aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu juu ya Mahakama kuzuia kuapishwa kwa mbunge mteule wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Julius Mtaturu.

Uamuzi wa Mahakama Leo hii ndio utatoa hatma juu ya Kuapishwa kwa Julius Mtaturu ambaye anatarajiwa kuapishwa hapo kesho.

Mnamo Agosti 26 Tundu Lissu alishinda pingamizi la serikali ya Tanzania ikiwakilishwa na mawakili 15 dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua kesi kupinga kuvuliwa ubunge wake chini ya Jaji Sirilius Matupa.

Lissu ambaye ni mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alifungua maombi Mahakama Kuu, Masijala ya Dar es Salaam chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai Lissu ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo kwakuwa mpaka sasa yuko nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 07, 2017 jijini Dodoma akitokea bungeni katika shughuli zake za kibunge.

No comments:

Post a Comment

Adbox