Rais John Magufuli amewataka watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi walioagizwa kuwasilisha barua zao za kuomba msamaha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) waamue wanamsikiliza nani kati ya Mawakili wanaotaka kuwachomoa pesa au DPP.
Ametoa kauli hiyo leo , alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kusamehe watuhumiwa hao wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali.
“Msamaha ukishautoa ni msamaha la sivyo wewe uliyetoa utaibeba hiyo dhambi kwa Mungu, ninafahamu wapo wanaodanganywa na mawakili wao ili waendelee kuwachomoa pesa wanaawambia ukiomba msamaha maana yake unakuwa umeshajishtaki mwenyewe sasa hiyo ni shauri yao waamue wanamsikiliza nani,” amesema Magufuli.
Aidha ameitaka ofisi ya DPP kuharakisha juu ya suala hilo ili watuhumiwa hao waweze kutoka wakajumuike na familia zao kutokana na sababu kuwa waliingia kwa njia ya mahaka hivyo wanapaswa kutoka kwa njia ya mahakama hivyo wawafikishe kwenye vyombo vya sheria ili waweze kuachiwa.
Monday, September 30, 2019
Kuweni makini na mnaowasikiliza - Rais Magufuli
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment